Kuhariri na iD
iD ni edita mpya (ilizinduliwa 2013) inayotumika kwenye mtandao ambayo inarahihisha kuhariri OpenStreetMap. iD inaharakisha halafu ni rahisi, na inakuruhusu kutengeneza ramani kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya data kama vile picha za satelaiti, GPS, Field Papers.
Edita ya iD ni njia kuu ya kuhariri wakati unataka kufanya mabadiliko madogo na rahisi, na kukukwepesha na utata wote ambao utaupata kwakutumia JOSM.
Yafuatayo chini ni utangulizi kwa kifupi kuhusu namna ya kutumia iD kwenye tovuti ya OpenStreetMap, ambapo unaweza kuifungua hatua kwa hatua na kukupa muongozo kwenye mambo muhimu baada ya kuingia kwenye tovuti ya OpenStreetMap.
Kufungua edita ya iD
- Kutumia ID utabidi uwe umeonganishwa kwenye mtandao.
- Tembelea tovuti ya OpenStreetMap katika http://www.openstreetmap.org.
- Login (Yingia) kwa kutumia akaunti yako ya OpenStreetMap
- Sogeza na kuza ramani yako paka kwenye eneo unalolitaka kufanya mabadiliko.
- Bonyeza kijimshale kidogo karibu na kitufe cha Edit (Hariri). Harafu bonyeza Edit with ID (in-browser editor) kama kwenye picha inayofuata.
Edita ya iD
Sehemu iliyobaki ya huu muongozo kwa sasa haipo. Bado inatafsiliwa.
Huu muongozo unapatikana katika Kiingereza au Kijerumani
Kusaidia kutafsili hii tovuti, nenda https://www.transifex.com na utafute HOT-OSM.